Hillary Clinton amehudumu katika nyadhifa nyingi siasa za Marekani, alikuwa mama wa taifa, seneta, waziri wa mambo ya nje. Sasa, anajaribu kwa mara ya pili kutimiza ndoto yake kuu, kuwa rais wa Marekani
Mwanasiasa huyu wa Democtratic wa umri wa miaka 68 alihudumu kama waziri wa mambo ya nje wa Rais Barack Obama mwanzoni mwa utawala wake Januari 2009.
Alijiuzulu muda mfupi baada ya Rais Obama kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili.
Ni mwanadiplomasia mashuhuri Marekani na anafahamika sana kwa kusafiri sana nchi mbalimbali na kufuata diplomasia ya kukutana ana kwa ana na wahusika.
Kuzoea kwake kufanya safari nyingi za kuchosha, kunamuandaa vyema kwa changamoto za safari nyingi za kampeni za urais.
Alijaribu mara ya kwanza kuwania urais lakini akashindwa na Rais Obama wakati wa mchujo wa chama cha Democratic mwaka 2008.
Hillary Rodham Clinton
- Alizaliwa 26 Oktoba, 1947 mjini Chicago
- Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Sheria cha Yale, 1973
- Aliolewa na Bill Clinton mwaka 1975
- 1993-2001: Alipigania kupanuliwa kwa bima ya afya na haki za wanawake alipokuwa mama wa taifa
- Alichaguliwa seneta wa New York mwaka 2000
- Alichaguliwa tena kwa kura nyingi 2006
- 2008: Alishindwa mchujo wa kuteua mgombea urais chama cha Democratic
- 2009-2013: Alihudumu kama Waziri wa mambo ya nje
Hillary Diane Rodham alizaliwa Oktoba 1947 mjini Chicago. Miaka ya 1960 alihudhuria masomo Chuo cha Wellesley jimbo la Massachusetts, na akaanza kujihusisha na siasa za wanafunzi.
Alisomea uanasheria katika Chuo Kikuu cha Yale ambapo alikutana na Bill Clinton. Walifunga ndoa 1975. Aliendelea kujihusisha na siasa baada ya Bw Clinton kuwa gavana wa Arkansas mwaka 1978.
Bw Clinton alipokuwa akifanya kampeni za urais mwaka 1992, alisema kwa mzaha kwamba alikuwa anawapa wapiga kura marais wawili "kwa bei ya mmoja".
Kama mke wa rais, Bi Clinto alitetea haki za wanawake na huduma ya afya kwa wote, na hilo likamuongezea sifa nyumbani n ahata nje ya nchi.
Hata hivyo, baada ya kushindwa kufanikisha mpango wa bima ya afya kwa wote, ambao hata haukujadiliwa katika bunge la Congress, wakosoaji wake wengi walimtazama kama mtu mwenye ndoto zisizoweza kutimia na limbukeni kisiasa.
Katikati mwa miaka ya 1990, wakati wa muhula wa pili wa mumewe Bill Clinton, alihusishwa na kashfa kadha zilizoathiri uongozi wake